Msanii wa Bongo movie na mwanamziki Sharo milionea amefariki dunia leo hii kwa ajali ya gari alipokua akielekea Muheza, Tanga., kwa habari zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa movie Steve Nyerere,
kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bwana Constatine
Massawe amesema " kifo cha Millionea kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa anaendesha gari aina ya toyota Harrier akitokea Dar kuelekea Muheza, alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka,na maiti imehifadhiwa katika chumba cha maiti ya hospitali teule ya Muheza. alikuwa mwenyewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi Amen..