Wednesday, 14 August 2013

LIFAHAMU KUNDI JIPYA LA BONGO FLAVA LILILOUNDWA NA AMINI & BARNABA

Wale wakali toka jumba la vipaji Tzee- THT walioishi kama pacha kwenye jumba hilo (Amini & Barnaba)
wameungana na kuunda crew yao mpya kimziki iitwayo “GEMENIH” wakimaanisha wao ni kama mwezi na nyota angani.
“Yap, Tumeungana kufanya kazi pamoja kama kundi nje ya THT tukiwa ni matunda ya THT na tumeamua kujiita hivyo kutokana na kutegemeana kwetu kwenye kazi na umuhimu wa uwepo wa kila mmoja kwenye mziki wa bongo kama umuhimu wa nyota na mwezi angani.” Barnaba alidokeza.
Kundi hilo kwa sasa lina-bang hewani na ngoma yao ya ‘Why me’ huku wakiwa na mipango mingi ya utendaji wao wa kazi kama Gemenih. Pia waliongeza kitu juu ya Gemenih na THT.
“Kikubwa ni kwamba, watu wasidhani tumetoka au tuna ugomvi na THT ila tumehitimu mafunzo pale na kutunukiwa vyeti nasi ni matunda ya THT na bado tunashirikiana nao kwa kuwapa ushauri hata kuwatungia nyimbo. Kwa ufupi tumewaachia wengine nafasi baada ya sisi kufuzu mafunzo pale.” Amini aliongeza.
Gemenih ipo chini ya meneja aitwaye Moses Clemence ambaye ndiye ana-control mambo yote yahusuyo vijana hao.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...