Tuesday, 24 December 2013

RJ COMPANY YATANGAZA NAFASI ZA KAZI.


Mwandaaji, Director ambaye pia ni muigizaji wa filamu za kibongo Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni ya ‘RJ’ akiwa na mwenzake anayejulikana kwa jina la Johari now wametangaza kuwa wanahitaji kuajiri watu wawili wenye vipaji vya kuigiza wenye kiwango cha elimu ya kidato cha nne ikiwa ni kama fursa ya kipekee katika kampuni hiyo.
“RJ Company tunatafuta watu wawili wenye vipaji vya kuigiza ili tuwaajiri, tunahitaji wenye elimu ya kidato cha nne lengo ni kutaka kuongeza mastaa wapya kwa kufanya kazi vizuri kupitia kampuni yetu” – Ray Kigosi.