Tuesday, 10 December 2013

Vituko vya kufunga mwaka: Lady Gaga atembea na mti wa X-mas kichwani!

Vituko bado anaviendeleza msanii wa muziki kutoka nchini Marekani Lady Gaga ambaye
ameonekana kuianza rasmi sikukuu ya X-Mass kwa kutembea na mti wa X-mass kichwani mwake.
Baadhi ya watu wengi wamezoea kupamba maua mbalimbali sebuleni na hata vyumbani kwao lakini kwa msanii huyo hali imekuwa tofauti ambapo yeye ameamua kuubeba mti huo kichwani mwake.