Tuesday, 25 February 2014

Kajala anusurika kifo baada ya kunywa kinywaji chenye sumu.

Jumapili ya tarehe 23 FEB 2014, kulikuwa na show ya izzo biznes pande za Kibo Complex tegeta ambapo
wasanii mbalimbali walikuwapo kumpa support izzo akiwemo Msanii wa Bongo movie, Kajala Masanja.
Kama alivyoelezea mwenyewe kupitia mitandao ya kijamii kuwa akiwa kwenye hiyo show ghafla akijihsi kuumwa ndipo kwenda hospitali ikabainika kuwa alikunywa kinywaji kilichowekwa sumu.
"Jana nilivyokuwa kwenye show ya Izzo ghafla nikaanza kuumwa nikapelekwa home alafu nikaenda hospita nilivyopimwa nikakutwa nimekunywa kitu chenye sumu lkn namshukuru mungu naendelea vizuri asante mungu kwa kila jambo" aliandika Kajala kupitia mitandao ya kijamii.