MSICHANA anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva Agnes Jerald maarufu kwa jina la (Masogange)
ni miongoni mwa wanawake waliotajwa kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, ambapo msichana mwingine aliyekamatwa ametambulika kwa jina la Melisa Edward.
Inadaiwa mabinti hao kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam , Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za
Alisema kuwa wawili hao walikamatwa mnamo tarehe 5 mwezi huo nchini humo, na bado wanashikiriwa na jeshi la polisi la nchini humo kwa ajili ya uchunguzi.
"Hadi sasa taalifa rasmi bado hazijafika hivyo, hatujajua ni aina gani ya adhabu wanaotumikia tunasubili taarifa rasmi kutoka huko" alisema Nzoa.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii zilidai kuwa jumapili iliyopita taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Kulevya, Geofrey Nzoa, alithibitisha kukamatwa kwa wasichana hao nchini huko ambapo aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald pamoja na Melisa Edward.