Sunday, 14 April 2013

HISTORIA FUPI YA MAISHA YA KIMUZIKI ya A.Y(Ambwene Yesaya)


Ambwene Allen Yessayah (amezaliwa tar. 5 Julai 1981Mtwara) ni mwanamuziki wa muziki aina ya Komesho, Rap na Hip Hop, Muigizaji na pia mwanamitindo kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina la AY. AY ametoa nyimbo nyingi maarufu nchini Tanzania, moja kati ya nyimbo hizo kama vile Raha tu 1-2, Raha Kamili, Machoni kama watu, Binadamu nk.
AY ambaye anafahamika sana
nchini TanzaniaKenyaUgandaRwandaBurundi hadi Kusini mwa Afrika. Vile vile alikuwa mwanakikundi wa East Coast Team linaloongozwa na Gwamaka Kaihula aliye maarufu kama King Crazy GK, na mwenzake Khamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Falsafa au Mwana FA. Kundi hilo la Muziki lina maskani yao Upanga jijini Dar es salaam.
Albamu Alizotoa
  1. Raha Kamili (2003)
  2. Hisia Zangu (2005)
  3. Habari ndiyo hiyo (2008)