MWANADADA mahiri kwenye maigizo na vichekesho nchini, Tumaini Martini ‘Matumaini’, anatarajia kuachia filamu yake mpya iitwayo The Dream hivi karibuni.
Matumaini amejizolea umaarufu kwenye tasnia hiyo kutokana na vituko vyake alipokuwa kwenye kundi la Kaole pamoja masnii mwenzake, Kiwewe.
Akizungumza na WATU SMART ENTERTAINMENT jana, alisema filamu hiyo itakuwa burudani kutokana na vituko vilivyomo ambapo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mwisho.
“Filamu hiyo itakuwa ya kipekee na haitawachosha watazamaji kutokana na kujaa vituko na mikasa vinavyotokea kwenye jamii yetu,” alisema matumaini.