Wednesday 3 July 2013

FID Q NDANI YA POETRY ADDICTION


MSANII wa mini anayeimba miondoko ya Hip Hop Faridi Kubanda 'Fid Q' , ni miongoni mwa wasanii wanaoandika historia ya muziki huo kwa kufanya shoo ya kwanza iliyopewa jina la Poetry Addiction lenye lengo la kupinga vita ujinga.



Shoo hiyo ambayo iliandaliwa na kampuni ya Cheusi Dawa ambayo ipo chini ya msanii huyo mwisho wa wiki hii jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali ambapo Mad Ice pamoja na Wakazi waliipamba shoo hiyo kwa kufanya shoo live jukwaani hapo.

Akizungumza baada ya shoo hiyo aliweka wazi kuwa, shoo kupitia shoo hiyo vijana wameweza kupata uelewa kwa kufanya muziki kama ajira kwa kuweka mikakati iliyothabiti ili kuboresha muziki huo.

Alisema tamasha hilo ambalo limetumia ala za muziki kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jamii na kuamini kuwa kila kijana ambaye aliweza kufika katika shoo hiyo ameweza kupokea ujumbe kuhusu swala zima la kutumia muziki kama ajira.

Fid Q ambaye anazidi kujiongezea umaarufu kuonekana tofauti pia kwa kufanya shoo hiyo ya Hip Hop 'live' kwa kuimba kwa kutumia bendi hali ambayo haijazoeleka sana kwa muziki wa aina hiyo kutumia bendi.

Hali hiyo imemuongezea msanii huyo mashabiki wengi huku akiwa katika nafasi nzuri ya kuutangaza muziki wake kimataifa kutokana na ubunifu na uwezo ambao anauonyesha.

Shoo hiyo ambayo imeshuhudiwa na wana Hip Hop na wasanii wengine ambapo baadhi ya wasanii waliotumbuiza usiku huo waliimba live hali ambayo inaonyesha muziki wa Tanzania umepiga hatua kwa kiasi kikubwa tofauti na hapo awali.