sasa.
Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, zilisema Brandts ameutaka uongozi kuhakikisha unamsaka Niyonzima kwa njia yoyote ile, ikiwezekana kutumwa mtu mmoja kumfuatilia nyumbani kwao Rwanda.
Hata hivyo, Brandts aliamua kumpa jukumu la kumfuatilia mchezaji huyo, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrance Mwalusako.
Kiongozi huyo alisema, kocha huyo alishangazwa na kutotokea kwa mchezaji huyo katika mazoezi yaliyoanza kufanyika juzi kwenye viwanja vya Loyola, kwani mara ya mwisho alikubaliana naye kuwa anatakiwa kuripoti mazoezini pindi timu itakaporejea jijini.
“Mwalimu alibainisha, alimruhusu Niyonzima kwa muda na walikubaliana angerudi nchini pindi timu nzima itakaporejea kutoka katika ziara zake za Kanda ya Ziwa,” alisema.
Alieleza mwalimu alipofika katika mazoezi ya jana, alishangazwa kutomuona Niyonzima, hali iliyomfanya kuhamaki na kuwataka viongozi wa timu kuhakikisha wanamtafuta mchezaji huyo.
“Mwalusako amepewa jukumu la kuhakikisha Niyonzima anarudi haraka, kwani hata mwalimu mwenyewe haelewi tena tatizo linalomfanya mchezaji huyo kushindwa kurudi nchini hadi sasa,” alisema.
Alisema tabia ya mchezaji huyo kuchelewa kuripoti mazoezini, imekuwa ni jambo la kawaida kila mara timu inapokwenda likizo, huku viongozi wakishindwa kumchukulia hatua yoyote.