Wednesday 7 August 2013

Don Jazzy aungana tena na D’Banj!

Patna wa zamani wa Mo’Hits Records, Don Jazzy and D’Banj wameonekana pamoja kwa mara ya kwanza tangu waachane mnamo March 2012.

Patna hao walikutana katika harusi ya dada  mdogo wa D’Banj ambaye alifunga ndoa na Dotun wa Cool FM jana, August 3, 2013 kwenye ukumbi maarufu wa The Grandeur Event Centre uliopo Ikeja mjini Lagos.
Don Jazzy ambaye ni produza mkali wa Mavin Records na D’Banj ambaye ni msanii machachari kutoka DB Records waliwapagawisha wageni waalikwa baada ya kuivamia steji na kuanza kuwarusha maharusi kwa nyimbo zao kali za ‘Mr Endowed‘, ‘Fall in love‘ and ‘Suddenly‘.
Japokuwa patna hao walishawahi kukutana mara kadhaa tangu waachane, hii ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuimba pamoja stejini tangu walipoachana.
D’Banj alielezea furaha yake ya kuungana tena na Jazzy pia aliwapa maharusi zawadi ya gari mpya na ya kisasa aina ya Honda CRV.
Uhusiano wa kimuziki wa Don Jazzy na D’banj ulivunjika bila ya kujulikana chanzo cha mgogoro huo mnamo mwaka jana.Watu waliokuwa lebo moja na washiriki kama Dr SID, D’Prince na Wande Coal walijiunga upande wa Don Jazzy wakati mdogo wake, KaySwitch alijiunga na D’Banj.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...