Saturday, 10 August 2013

Gervinho akamilisha usajili AS Roma

Winga Mshambuliaji wa Ivory Coast,Gervais Lombe Yao Kouassi maarufu kama Gervinho amekamilisha uhamisho wa kuichezea As Roma ya Italia.

Uhamisho huo wa Gervinho umetajwa kuwa wa pound milioni 8 walizopewa Arsenal.
Gervinho alihamia Arsenal mwaka 2011 akitokea Lile ya Ufaransa.
Msimu wake wa kwanza aliifungia Arsenal magoli manne kabla ya kufunga magoli saba msimu uliopita.
Amekuwa akipata ushindani wa kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger, na huenda usajili wake wa kuhamia Seria A utakuwa changamoto mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...