Sunday, 11 August 2013

Man United yanyakua Community Shield

Meneja mpya wa United Moyes alitumia muda wake mrefu katika mazungumzo juu ya hatma ya mashambuliaji Wayne Rooney,lakini uwanjani amekuwa
mshambuliaji Van Persie aliyefunga magoli mengi msimu uliopita ambaye tena ameiwezesha timu hiyo kuibuka mshindi.
Mchezo ulipoanza, imemchukua dakika 6 tu Van Persie kunusa nyavu kwa kuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na mlinzi wa kushoto, Patrice Evra.
Wigan ambayo sasa inacheza katika daraja la pili,imejaribu kutishia ngome ya United bila mafanikio kwani walinzi wake walionekana kudhibiti vilivyo sehemu zao uwanjani.
United walijihakikishia kuondoka na ushindi kunako dakika ya 59 ambapo pia amekuwa mshambuliaji Van Persie aliyetikisa wavu kwa mkwaju wake uliopiga kwenye mguu wa mlinzi wa Wigan na kumhadaa mlinda lango.
Ushindi huo wa Manchester United wa magoli 2-0 ametosha kwa meneja mpya David Moyes kusherehekea kombe la community Shield,kombe lake la kwanza.
Baada ya ushindi huo sasa macho yanaelekezwa upande wa ligi kuu ambapo United wataanza kampeni ya kutetea taji lao ugenini dhidi ya Swansea siku ya jumamosi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...