Thursday 5 September 2013

PROFESA JAY AFUNGUA STUDIO


MSANII mahiri wa muziki wa Kizazi kipya nchini, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, amefungua studio ya kuandalia muziki ili kusaidia wasanii wanaochipukia. Studio hiyo ambayo bado haijapatiwa jina, iko Msasani, jijini Dar es Salaam na itakuwa inapokea wasanii wenye vipaji mbalimbali, wakiwemo wa muziki wa hip hop, Reggae, taarabu na hata wale wanaopenda kujifunza kupinga vyombo.

Akizungumzia swala hilo, Profesa Jay alisema ameamua kufungua studio hiyo kama kutoa shukrani kwa mashabiki kwa kumsapoti katika muziki tangu alipoanza hadi sasa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...