Tuesday, 31 December 2013

Agnes Masogange kuonekana katika video ya Tunda Man "MSAMBINUNGWA"


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Khalid Ramadhani Tundamani anatarajia kumwonyesha kwa mara ya kwanza 'Video queen' Agnes Gerad maarufu Masogange katika video ya wimbo wake wa Msambinungwa.

Akiongea Tundaman alisema ataondoka nchini Januari 5, 2014 kwenda Nairobi kwa ajili ya utengenezaji wa Video hiyo na kwamba ameamua kufanya video hiyo akiwa na Masogange kwani ni msichana anayefanya vizuri katika video nyingi za wasanii pia ana kipaji cha kazi hiyo.