Saturday, 28 December 2013

Jackie Cliff akamatwa na dawa za kulevya nchini China.


Mwana dada mrembo maarufu kwa jina la Jackie Cliff, ambaye wasanii wa hapa nchini hupenda kumtumia mrembo huyo katika kazi mbali mbali za entertainment … sana sana katika music videos; imeripotiwa kuwa mrembo huyu anashikiliwa na uwongozi wa kisheria nchini China baada ya kubainika kuwa anajihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya…

Kupitia mitandao mbalimbali habari zimezagaa kuwa kuna mwanamke, amekamatwa nchini China katika jiji la Macau na kilo 1.1 za heroin alizokuwa amezihifadhi tumboni kwake, lakini jina mwanamke huyo halikutajwa na wala hakuweza kutambuliwa kutokana na picha zilizopigwa za mrembo huyo wakati amekamatwa zimepigwa akiwa amefunikwa uso na mask nyeusi.

Lakini habari za hivi karibuni zinasema msichana huyo anaweza kuwa ndiye mrembo Jackie Cliff kutokana na habari kutoka kwa Star wa bongo aliyekataa kutajwa utambulisho wake, ambaye na yeye yupo huko nchini China kuthibitisha kwa kusema kuwa mwanamke aliyekamatwa na vidonge hivyo vya Heroin ni mrembo Jackie Cliff.