Friday 7 March 2014

Huu ndio ujio mpya wa Mfalme wa Rhymes "AFANDE SELE"

Moja kati ya studio ambayo inafanya vizuri katika utayarishaji wa muziki jijini dar es salaam
sinza lego Flexible music imekuja tena na Mfalme wa Rhymes Afande Sele na ngoma yake mpya inayoitwa Mwendo kasi aliyoifanya katika studio hizo.
Mwendo kasi ni ngoma ambayo inaelezea ajali mbali mbali zinazotokea barabarani ambazo zinasababishwa na uzembe wa madereva na kusababisha vifo vya wananchi, akiwa amewashrikisha wasanii kutoka mkoani Morogoro Dyna Nyange na Ballet.
Pia wimbo huo ambao umetengenezwa na mtayarishaji kutoka Flexible Music anayeitwa Mbatizaji akiwa ameutengeneza kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na vyombo na ubora wa studio, hata hivyo katika wimbo huo ambao umefafanua mambo mengi yatokeayo barabarani.
Kwa mashabiki wa Afande Sele mkae tayari kwa kile kitu ambacho amekizungumza katika wimbo huo maana amezungumza mengi  kama unavyojua Mfalme wa Rhymes huwa akitoa kitu hakosei kwa mashabiki wake.
Katika wimbo huo amewazungumzia kwa wale madereva ambao wanakunywa pombe kisha wanaingia barabarani kumata uskani na kuendesha gari kwa mwendo wa kasi na kusababisha ajali pia ameongea kuhusu abiria ambao wanakaa kimya wakati dereva akiwa anaendesha gari kwa kasi.
Na Pia kwa madereva ambao wanaongea na simu huku wanaendesha magari, pia ku overtake katika kona kali maana nao wanaweza kusababisha ajali na kupoteza uhai wa binadamu maana uhai hauji mara mbili.