Saturday, 13 July 2013

MCHEZAJI KUTOKA KENYA ATUA ENGLISH PREMIER LEAGUE

Southampton imemsajili mcheza kiungo wa Celtic Victor Wanyama (MKENYA)
kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili na nusu
.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye alijiunga na Cletic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, amesaini mkataba wa miaka minne na Southampton.
Wanyama, kutoka Kenya, aliteuliwa kuwa mchezaji bora mchanga katika ligi ya Scottland mwaka uliopita na alifunga bao wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Barcelona ambayo Celtic iliibuka na ushinda wa goli moja kwa bila.
Kiasi hicho ndicho cha juu zaidi kwa mchezaji yeyote kuuzwa nchini Scottland.
Wanyama vile vile amevunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Kenya kushiriki katika ligi kuu ya Premier ya England.