Sunday, 23 June 2013

''YEEZUS'' YA KANYE WEST YAIFUNIKA ''BORN SINNER'' YA J.COLE


Kutokana na kitengo (First week projections sales) kinachoangalia mauzo ya albamu,albam ya Kanye West “Yeezus” inaongoza. Albamu ya Kanye West “Yeezus” na ya J.Cole “Born Sinner” zimetoka siku
moja tarehe 18/6/2013 Jumanne. J.cole anaweza asipende ripoti ya mauzo ya wiki ya kwanza lakini wao ndo wakali wanaongelewa sana wiki hii katika ulimwengu wa Hip Hop. Billboard wametoa ripoti mpya kwa wiki hii ikimweka Kanye West juu akiongoza. Kutokana na ripoti hiyo albamu ya Kanye West Yeezus itaongoza kwa copies 360,000 – 380,000 zilizouzwa. Kama ilivyotarajiwa na wengi mapema mwezi huu J.cole amefuatia kwa copies 150,000 – 200,000. Lakini J.cole alisema kupitia Twitter kwamba hajapenda ripoti ya mauzo ya wiki ya kwanza akasema wanaiendesha hip hop.