BAADA ya kuugua homa ya matumbo ‘Typhoid’, daktari anayemtibu msanii Seleman Msindi ‘Afande Sele,
ameshauri msanii huyo afichwe sehemu tulivu ili aweze kupona. Daktari huyo alimwambia msanii huyo, baada ya kutoka hospitalini alikokuwa amelazwa akitakiwa kutumia muda mwingi kulala ili apumzike.Hivyo kutokana na ushauri huo msanii huyo anayeshikilia taji la mfalme wa ‘rhymes’, kipindi chote cha ugonjwa atakuwa anaishi kwa kaka yake Ali Msanii, Kigurunyembe mkoani Morogoro.
Afande Sele alisema dalili za magonjwa yanayomsumbua alianza kuisikia akiwa Mwanza, lakini alipuuza kwa kunywa Panado na aliporejea Dar es Salaam, ndipo akazidiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
“Nikiwa Mwanza nilianza kutapika na kujihisi vibaya nikanywa Panado ila niliporejea Dar es Salaam hali ikawa mbaya nikalazwa na daktari ameniambia nisizungumze sana na sitakiwi kukaa kwenye kelele,” alisema Afande Sele.