KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Parklane la mkoani Tanga, lililowahi kutamba katika muziki huo, linatarajia
kusukwa upya baada ya kutofanya kazi pamoja kwa muda mrefu. Kundi hilo liliwahi kutamba na wimbo wake kama ‘Nafasi nyingine’ uliorekodiwa Studio za Tabasamu Records ya Mombasa nchini Kenya.
Akizungumzia ujio huo, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Ismail Sadiq ‘Suma Lee’ amesema wanatarajia kurejea upya na wataachia wimbo wao mpya wa ‘Kila mtu na wake’.
Suma Lee alisema malengo yao kwa sasa ni kuhakikisha wanatoa nyimbo kali ambazo zitawafanya mashabiki wao kuendelea kuwakubali kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya kusambaratika.