Friday, 2 August 2013

Juma Kaseja asaini rasmi FC Lupopo

HATIMAYE aliyekuwa kipa wa Simba SC na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Juma Kaseja amesaini kuichezea klabu ya FC Lupopo ya Jamhuri ya
Demokrasia ya Congo (DRC), kwa miaka miwili.

Kaseja amesaini jana kwa dau la Sh milioni 50 kuichezea klabu hiyo na sasa atakuwa anasubiri Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili aweze kuondoka nchini Jumanne kuelekea mjini Lubumbashi tayari kuitumikia klabu hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA Meneja wa timu hiyo, Balanga Ismael, alisema tayari wamemalizana na Kaseja baada ya kumaliza taratabi zote ikiwemo mambo aliyokuwa akitaka kipa huyo.

“Mchezaji mwenyewe ameridhia kujiunga nasi, tunaamini hadi atakuwa tegemeo kwetu na tunafurahi sana kuwa naye kikosini,” alisema.

Alisema Kaseja atakuwa ni chaguo lao la kwanza kwenye kikosi cha FC Lupopo.