Tuesday, 8 October 2013

Haya ndiyo yanayoendelea kumuhusu RAY C na kazi za muziki anazofanya.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamira ‘Ray C’, ameanza kusaka jina la kuipa albamu yake
mpya,
itakayobeba nyimbo zaidi ya 10. Ray C aliliambia gazeti la RAI Jumatatu, kuwa hatafanya haraka kuchagua jina sahihi litakalopendezesha albamu hiyo, kwani anatambua mashabiki watasubiri kuona vitu vizuri alivyoandaa baada ya kuwa nje ya gemu muda mrefu.
Msanii huyo aliongezea amejitahidi kuwashirikisha wasanii mbalimbali, ambao wana majina makubwa na vipaji vya hali ya juu hapa nchini.

“Wasanii wengi nimebahatika kuwashirikisha kwenye albamu hii, wengi vijana tena wamebarikiwa sauti nzuri na vipaji,” alisema Ray C.

Hata hivyo Mwanadada huyo hakuweka wazi kama amefanikiwa kufanya wimbo na msanii wa THT Recho, ingawa alisema hiyo ni siri yake na itakuwa kama ‘surprise’ kwa mashabiki.