Sunday, 13 October 2013

Hii ndio kazi inayokuja kutoka kwa WAKAZI.

MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Webiro Wassira ‘Wakazi’, anatarajia kuachia video ya wimbo wake
mpya wa ‘Touch’ wiki ijayo. Akizungumza na RAI jana, Wakazi alisema video hiyo ipo katika maandalizi ya mwisho na tayari inatarajiwa kuwa hewani ili mashabiki waweze kuiona.

Wakazi aliwashukuru Watanzania kwa kuzipokea kazi zake mbalimbali vizuri, akiwa na matumaini makubwa ya kufanya mabadiliko kwenye tasnia ya muziki wa Hip Hop.

“Nimejipanga kuleta mabadiliko katika ulimwengu wa muziki, ninaanzia hapa nyumbani, matumaini yangu ni kufanikiwa kimataifa,” alisema. 

Wakazi amewahi kufanya shoo katika jumba la Big Brother mwaka huu na ameanza kufanya vizuri katika muziki.