Saturday, 12 October 2013

Jaji Hermy B awashauri watanzania kuhusu Tusker Project Fame.

Baada ya kuwafahamu majaji wawili wa TPF6 ambao ni Ian Mbugua (Kenya) na Juliana Kanyomozi (Uganda),
hatimaye
jina la jaji wa tatu limefahamika ambapo C.E.O wa BHitz Music, Hermes Bariki a.k.a Hermy B (Tanzania) ndiye atakayeungana na majaji hao wawili.
Akiongea na 100.5 Times fm Hermy B amewashauri watanzania kuwasapoti washiriki wanne kutoka Tanzania kwa kuwapigia kura kwa kuwa ushindi hutokana na wingi wa kura anazopigiwa mshiriki na sio anachosema jaji.
“Watanzania wasifikirie kwamba Jaji wao ndiye atakayewapatia ushindi washiriki wao, ndio wapige kura sasa, kwa sababu ushindi wa watu wengi unatokana na kura na sio jaji, hata Juliana akimwambia you are the best of the best lakini asipopigiwa kura hawezi kushinda.” Amesema Hermy B.
Washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika TPF6 ni Angella Karashani a.k.a Angel, Tanah, Hisia na Dubson.
Mshindi wa mwaka huu atapewa shilling Million Mia Moja, na mkataba wa kurekodi nyimbo kwa gharama ya shilingi Million mia mbili za Tanzania.