Saturday, 12 October 2013

Raheem kujumuishwa katika kikosi cha England kitakachovaana na Poland.

Winga wa Liverpool FC Raheem Sterling ameitwa katika kikosi cha England
ambacho kitapambana na Poland siku ya jumanne katika uwanja wa wembley katika kuwania tiketi ya kushiriki fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil.

Hii imetokana na kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson kuwakosa wachezaji wake Tom Cleverley na Kyle Walker .