Tuesday 25 February 2014

KALAMU YA NIKK WA PILI: SANAA SIO UTAMADUNI, NI BIASHARA.

Imeandikwa na Nick wa Pili

Katika makala yangu iliyopita nilijaribu kutafakari juu ya thamani ya sanaa, tafakari ya makala ile ili kosa msingi wa kifalsafa ambao ni kujuwa kiini cha ndani cha jambo husika. Ushahidi unaonesha kuwa kiini kinacho itafuna sanaa ya tanzania..ni kanuni na mtizamo,


Kwakuwa hoja hii ni pana na ngumu kidogo.. Nimechaguwa namna Moja ya kipekee kuielezea kiufupi ili iweze kueleweka, hoja hii itaongozwa na Msemo maarufuu..

JE! WAJUWaaaa….???
Sisi Soko letu la muziki ni kubwa kuliko la kenya lakini wao Mwaka jana wamekusanya 
mirabaa shilingi billioni 10 wakati COSOTA wao kiwango kikubwa walichowahi kukusanya kwa muda wa mwaka mmoja ni shilingi milioni 380.
Familia ya marehemu Kanumba haimiliki wala haitafaidika na movie 44 ambazo marehemu alizitengeneza wakati wa uhai wake, wakati Whitney Houston familia yake imefaidika sana kwani baada ya kifo chake ameuza nakala nyingi sana za CD.
Kuna haramia mmoja alikamatwa na mzigo haramu wa muziki na bongo movies wenye thamani ya shilingi millioni 200, lakini alipo fikishwa mahakamani faini yake haikuzidi shilingi milioni 5, na hapo sheria ilifuatwa kikamilifu haswaa bila kupindishwa
Haramia mwingine wa muziki na bongo movies mfanyabiashara wa Kariakoo na mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye hufunguwa biashara yake saa tisa usiku na kuifunga saa kumi na moja alfajiri yaani yeye anafanya kazi kwa muda wa masaa matatu tu…polisi walipo mkamata nyumbani kwake aligundulika kuwa na utajiri mkubwa na alikuwa akiishi maisha ya kifaharii ambayo msanii hawezi kuyaota hata kwa ile ndoto ya usiku
Je, wajua creative industry (yaani tasnia ya ubunifu wa kisanaa unaotegemea akili unao julikana pia kama mali isiyo shikika (non tangible asset) nchini Tanzania umechangia pato la ndani la taifa kiasi cha shilingi billion 680 kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi mwaka 2010, na kuishinda sekta ya nishati na madini, lakini wafanyakazi wa sekta hiyo pato lao halikuongezeka…na wala ulinzi wa ubunifu haujawahi kuwa haki ya kikatiba katika mika 50 ya uhuru wa Tanzania, wala haijatajwa katika rasimu ya katiba mpya?
Vijana milioni 6 wanajihusisha na sanaa, na ajira yao kuwa kama moja ya ajira duni, na wala hawajatambuliwa wala kutajwa katika rasimu ya katiba itakayoanza kujadiliwa kama kundi maalumu kama yalivyo tambuliwa makundi mengine ya wavuvi, wakulima n.k.
Sanaa ya Tanzania inapovuka mipaka haina ulinzi kwa sababu Tanzania sio mshirika wa taasisi za kimataifa za ulinzi wa kazi za sanaa kama WCT na WIP…kazi za kisanaa za kitanzania zimezagaa kuanzia ukanda wa Afrika Mashariki, Ulaya, Asia, America (unprotected) na matumizi ya kazi hizo kutokuwa na manufaa kwa wahusika.
Ukitizama kwa makini mambo mbali mbali niliyo ya bainisha katika aya zilizotangulia utagundua kuwa sanaa ina manufaa na ina thamani katika uhalisia(in practice) lakini kikanuni hapana, kwa maana hakuna kanuni za kusimamia manufaa hayo na thamani hiyo kwa ustawi wa Sanaa na wasanii.
Msingi wa hayo yote ni mtizamo wa kiserikali (kitaifa) kuitizama sanaa kama sehemu ya utamaduni tu, na sio kama sehemu ya kiuchumi, biashara, ajira na maendeleo.
Mtizamo huu umepelekea kukosekana kwa sera, sheria, kanuni na taasisi za kusimamia na kutengeneza mazingira bora ya ustawi wa tasnia hii.
Sio sahihi kutizama sanaa Kama utamaduni katika mfumo huu wa sasa wa maisha ambapo soko na mitaji ndio vinaongoza dunia…mfano muziki ni biashara kubwa, thamani yake kwenye soko la dunia ni US$ 36.9 billion. India ambako muziki ni sehemu kubwa ya utamaduni wametambua hilo na sasa ni nchi ya pili kwa kuuza muziki duniani thamani ya soko lao ni US$ billion 5.
Matokeo ya mtazamo huu wa kuitizama sanaa kama sehemu tu ya utamaduni umesababisha kumekosekana, uwekezaji, tafti, takwimu, ufahamu, ueledi, usimamizi, ulinzi wakisheria kulinda haki za kiuchumi za msanii. Na kuwa na mipango iliyo kosa ueledi wa sanaa..mfano Stika za TRA kwa ajili ya kodi kwa CD zinazouzwa mitaani, huu ni mtazamo finyu, muziki unatakiwa ulindwe popote ulipo (copyright) sio kwenye CD tu zinazo uzwa…VIP, mabaa, majumbanii, mtandaoni, Kwenye media, vyombo vya kieletroniki, saloon, matangazo, nk.
Hoja ya msingi itakayoweza kuvunja mtazamo huu uliozaa mazingira haya mabovu ni kwa wasanii kutambulika kikatiba na kuingizwa na kutambulika kwa haki bunifu (intellectual property right) katika katiba…..haya yatawezekana kwa kupitia wabunge wa bunge la katiba kuingiza mapendekezo hayo ambayo hayakutajwa katika rasimu ya katiba.
Ikumbukwe kwamba katiba hii ikisha pita ndio basi, ni labda mpaka miaka 50 ijayo.
Toa maoni yako nini kifanyike kuingiza mapendekezo haya Katika mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba na wewe utafanya nini kufanikisha jambo hilo.
Hoja kuu ni wasanii kutambulika kikatiba na pili ni kutambulika kwa haki bunifu ( intellectual property right) kikatiba.
Niandikie katika kurasa zangu insta..nikkwapili , twitter nickmweusi@nikkwapili
Data nimezipta toka, utafiti wa shirika la WIPO..ulio dhaminiwa na serikali ya Tanzania.
Utafiti wa shirika la kimataifa la kazi duniani ILO.
Shirikisho la filamu Tanzania.
Mpango mkakati wa UNESCO Tanzania 2012.