Wednesday 26 February 2014

SHAZAD IQBAL YAIJIA JUU ‘DARK HOSE’ YA KATY PERRY NA KUITAKA YOU TEBE IITOE HEWANI…

Video ya wimbo wa Katy Perry ‘Dark Horse’ akiwa amemshirikisha Juicy J, imekumbwa
na msala baada ya taasisi ya dini ya kiislamu ya Uingereza inayojulikana kama Shazad Iqbal kutaka video hiyo iondolewe YouTube kwa madai ya kumkashfu Mwenyezi Mungu.
Taasisi hiyo imedai kuwa kipande cha video hiyo kinachomuonesha mtu akiwa amevaa cheni iliyoandikwa ‘Allah’ yaani Mungu, akishindwa na nguvu za giza (Magic Power) za Katy Perry aliyetamba kuzitumia kwenye wimbo wake. Lakini kibaya zaidi katika dakika ya kwanza na sekunde kumi na tano ya video hiyo, mtu huyo anaonekana akichomwa moto na kuuawa.
Taasisi hiyo imeiandikia ‘petition’ YouTube na tayari maombi hayo yameshakusanya sahihi zaidi ya 40,000 kwenye mtandao.
“Tunatumaini kwamba video yenyewe yenye picha hiyo itatolewa. Kitendo hicho hakisameheki na hakivumiliki, tunatumaini YouTube itaiondoa video hiyo.” Ameeleza mmoja wa viongozi wa taasisi hiyo.

Wimbo wa Dark Horse wa Katy Perry umeshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard 100 kwa wiki nne mfululizo na wimbo huo unapatikana katika albam yake inayoitwa ‘Prism’.