Sunday 28 July 2013

Leo ni birthday ya Johari (Blandina Chagula) huu ujumbe huu kwa mashabiki wake wote

Leo mwanadada Blandina Chagula maarufu kama Johari anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Tuliweza kupata
nafasi ya kufanya interview na mlimbende huyu katika siku yake hii kubwa ya leo ambapo pamoja na mambo mengi alitoa ujumbe huu kwa watu wote ma mashabiki wake wote.
“Napenda kuwaambia wapenzi wa filamu nchini kuwa kwanza kabisa nashukuru kwa support yenu kwa kununua kazi za nyumbani, kwani bila ninyi Johari asingekuwa Johari anayeonekana sasa. Napenda kuwashukuru wazazi wangu walionizaa kwani bila wao nisingefika hapa nilipo leo na pia mashabiki wangu wasipate wasiwasi kwani kila siku tunzaidi kupata mawazo mapya ya kuboresha filamu zetu hivyo wakae tayari kupata burudani zaidi na zaidi toka kwetu. Asanteni Sana”
Hongera sana dada Johari kufikia siku ya leo. Mungu akupe miaka mingi hapa Duniani.