Sunday 28 July 2013

Ushindi wa kwanza Hamilton kwa Mercedes.

Dereva wa magari ya Timu ya Mecedes Lewis Hamilton ameweza kuishindia timu yake ushindi wake binafsi wa
kwanza kwa Mercedes kwa kuongoza tangu mwanzo na kuwazidia madereva wenzake kwenye mashindano ya Hungary ya mbio za magari ya Langalanga au Formula 1.
Hamilton alijituliza na kutumia kasi akiwashinda dereva Kimi Raikkonen wa Timu ya magari ya Lotus aliyemaliza wa pili na Sebastien Vettel wa Red Bull aliyemaliza wa tatu.
Mark Webber wa Red Bull alionyesha umahiri wake kwa kujikwamua kutoka nafasi ya kumi alikoanzia mashindano hadi kumpiku dereva moto moto wa Timu ya magari ya Ferrari, Fernando Alonso.
Kutokana na hali hio Raikkonen sasa anapanda kwa pointi moja mbele ya Alonso akishika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi alizokusanya tangu kuanza kwa mashindano ya msimu huu wa 2013/2014 ingawa bado yuko nyuma ya kiongozi wa mashindano na mtetezi wa taji Sebastien Vettel kwa pointi 38.
Kwa kipindi kirefu cha mashindano haya Fernando Alonso alikua katika jitihada za kuzuia asipitwe na Romain Grosjean wa timu ya Mercedes, na katika pilikapilika Romain Grosjean, alijitia matatani na kuadhibiwa kwa kupita gari akizunguka nje ya uwanja.
Wakati huo alimpita Felipe Massa wa Ferrari kwenye mzunguko wa 29 kituo cha nne, ambapo tairi zote nne zilivuka msitari mweupe unaobainisha uwanja na papo hapo kupewa adhabu ya kuuzunguka uwanja.
Hapo jana baada ya Hamilton kushinda nafasi ya mbele ya kuongoza mbio za leo alisema kua utakua muujiza endapo atashinda ikizingatiwa hali ya joto kali nchini Hungary bila kusahau matatizo yaloikumba timu ya magari ya Mercedes kwa matairi kupasuka kila mara.
Lakini alidhibiti mashindano kwa mda wote akipoteza uongozi kwa Grosjean na baadaye Mark Webber aliposimama kubadili tairi na mafuta lakini aliweza kurudi kileleni pale Webber aliposimama kubadili tairi na mafuta.