Friday, 2 August 2013

LINA AZUNGUMZIA UJIO WAKE WA KIZOMBA

MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) Linah Sanga, amekamilisha wimbo wake mpya wa Kizomba.


Akizungumzia wimbo huo, Linah amesema wimbo huo wenye mahadhi ya Zuku utakuwa hewani mwanzoni mwa Septemba katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

“Wimbo huu ni moja ya nyimbo nilizofanya kwa mtayarishaji kutoka nchini Comoro, Johban Joh, ambaye yupo nchini kwa kazi maalumu, hivyo nimeamua kuongeza vionjo vya kutoka tamaduni za kwao ili kupanua wigo wa muziki wangu,” alisema Linah.

Alisema kwa sasa anahakikisha anaachia nyimbo nyingi kali kwa ajili ya mashabiki wake ambao watafurahi.