Friday, 2 August 2013

Linex kupiga kazi na Ney wa Mitego

MSANII wa muziki wa Kizazi kipya, Sunday Mangu ‘Linex’ anatarajia kufanya kazi mpya na Ney wa Mitego. Akizungumza na WATU SMART ENTERTAINMENT jana, Linex
alisema ingawa staili ya muziki anayoifanya, haifanania na Ney wa Mitego, lakini anafikiria namna ya kuanda wimbo huo.

“Nahitaji kufanya kazi na Ney wa Mitego, lakini yeye anafanya muziki wa Hip Hop, hivyo nina kazi ya kuhakikisha wimbo ambao tutaufanya unakuwa bora zaidi,” alisema.

Linex mbali na kufanya kazi na Ney wa Mitego, amepanga kufanya shoo katika mikoa mbalimbali nchini baada ya kumalizika mwezi wa Ramadhan.